Frequently Asked Questions

1. Mradi wa SafariCity unapatakana wapi?

Mji huu upo katika kitongoji cha Mateves, km 3 kutoka uwanja wa ndege wa Arusha, km 10 kutoka Arusha mjini na km 50 kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

2. SafariCity ni nini?

SafariCity ni mradi wa kitovu cha mji wa kisasa jijini Arusha unaoendelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Mradi huu unaendelezwa katika eneo lenye ukubwa wa ekari 563.4 na umepangiliwa kitaalamu kwa kuzingatia sheria za mipango miji.

3. Kitovu cha Mji ni nini?

Ni Mji mdogo ulio karibu na Mji mkubwa unaojitosheleza kwa mahitaji yote muhimu. Vitovu hivi hubuniwa na kuendelezwa ili kupunguza msongamano katikati ya miji mikubwa pamoja na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.

4. Lini ujenzi wa mji mzima utakamilika?

Uendelezaji wa Vitovu hivi vya miji ni wa muda mrefu kwa kuwa unalenga kukidhi ujenzi wa majengo ya aina tofauti tofauti kama vile makazi, biashara, ofisi na huduma za jamii. Majengo haya yanategemewa kuendelezwa na NHC, wawekezaji binafsi, taasisi binafsi na za serikali. Hivyo kukamilika kwa mradi huu kunategemea kiwango cha uwekezaji katika mradi huu.

5. Mradi wa SafariCity unajumuisha nini?

Mradi wa SafariCity unatoa fursa za uwekezaji katika viwanja/maeneo mbalimbali kwa watu binafsi, taasisi za serikali na taasisi binafsi. Uwekezaji wa viwanja hivi umegawanyika katika makundi yafuatayo:

6. Nini kinauzwa kwa sasa katika mradi wa SafariCity?

Wakati Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) likiendelea na utekelezaji wa mradi huu, NHC inawaalika watu binafsi pamoja na taasisi mbalimbali kununua viwanja kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Viwanja hivi vina ukubwa wa kuanzia mita za mraba 300 mpaka 3,000.

7. Punguzo la asilimia 40 la bei ya viwanja katika mradi wa SafariCity linawahusu wateja gani?

Punguzo la asilimia arobaini (40%) katika mradi wa viwanja wa SafariCity linawahusu wateja wapya wa viwanja. Wateja watakaonunua viwanja kuanzia tarehe 1/1/2020.

8. Punguzo la 40% linahusu viwanja gani?

Punguzo la asilimia arobaini (40%) linahusu makundi yote ya viwanja vyote vinavyopatikana katika mradi wa SafariCity. Viwanja hivi ni vya makazi, vya biashara, vya viwanda vidogovidogo, viwanja vya shule pamoja na taasisi za dini.

9. Bei mpya za viwanja ni zipi?

Bei mpya za viwanja ni

10. Je, punguzo hili la bei ni la muda gani? Ofa hii ina ukomo?

Punguzo la bei ya viwanja linalotolewa na NHC halina ukomo.

11. Je, kutokana na punguzo hili utaratibu wa malipo (Payment Plan) umebadilika?

Pamoja na punguzo la bei ya viwanja, utaratibu wa malipo haujabadilika. Wateja wa viwanja katika mradi huu bado wana fursa ya kulipa kidogokidogo kwa muda wa miaka 3-5 bila riba yoyote mara baada ya kulipa malipo ya awali ya asilimia ishirini na tano (25%).

12. Je, punguzo la 40% linawahusu wateja gani?

Punguzo hili linawahusu wateja wapya wa viwanja katika mradi wa SafariCity.

13. Je, wateja wanaoendelea na malipo ya viwanja vyao wanaruhusiwa kuomba refund (kurejeshewa fedha zao) na kuomba upya kununua viwanja kwa bei ya punguzo?

Wateja wanaoendelea na malipo ya viwanja vyao hawataruhusiwa kuomba kurejeshewa fedha zao kwa lengo la kuomba kununua viwanja kwa bei ya punguzo. NHC kwa kuwajali wateja wake imetoa punguzo la 10% kwa kiasi (deni) kilichosalia kwa wateja wake wanaoendelea na malipo ya viwanja vyao na watatakiwa kumaliza malipo hayo ndani ya miezi 6.

14. Nani anastahili kununua kiwanja katika mradi wa SafariCity?

Kila raia wa Tanzania anaruhusiwa kununua viwanja vya SafariCity. Raia wenye chini ya miaka 18 wanaweza kununua viwanja kupitia walezi/wasimamizi wao. Aidha, wawekezaji wasio raia wanaweza kuwekeza katika mradi huu kwa kufuata utaratibu utakaotolewa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (Tanzania Investment Centre).

15. Kuna faida gani za kuwekeza katika mradi wa SafariCity?

16. Nawezaje kununua kiwanja katika mradi wa SafariCity?