Bora, zinavutia, bei nafuu na rahisi kumiliki zaidi ya unavyofikiria!

NHC inajivunia kuwaletea nyumba za bei nafuu zilizoko ndani ya eneo tulivu la Kibada. Kigamboni Housing Estate ipo Kigamboni katika eneo linalofikika kirahisi, kilomita 17 kutoka Feri. Kigamboni Housing Estate ni mradi wa nyumba 182 zilizopangwa kwa kuzingatia vigezo vya miji ya kisasa yenye huduma za msingi zikiwemo sehemu za kuchezea watoto na shughuli mbalimbali za jumuiya, barabara pana inayotoa fursa kwa watembea kwa miguu na baiskeli kuwa huru vilevile, imezingatia nafasi ya miundombinu kama vile mitaro na umeme.

 

Nyumba hizi zenye vyumba viwili na vitatu ni mwanzo tu wa miradi mbalimbali inayoendelea nchi nzima. Uzinduzi wa Mradi huu ni chachu na dhamira ya Shirika la Nyumba la Taifa kuhakikisha watanzania wanapata nyumba bora na za kisasa vile vile zikiuzwa kwa bei nafuu. Wanunuzi wa nyumba hizi wataishi kwenye maeneo kwa kuzingatia mfumo wa hati pacha (Unit titles Act 2008). Mfumo huu utawawezesha wakazi kuishi katika utaratibu wakiongozwa na sheria hiyo ambayo imeundwa kulinda maslahi ya kila mnunuzi.

 

Kigamboni Housing Estate ina nyumba za aina mbili, nyumba ya vyumba vitatu na vyumba viwili. Nyumba ya vyumba vitatu ina ukubwa wa 70m² huku nyumba ya vyumba viwili ikiwa na ukubwa wa 56m²

 

Kila nyumba inajitegemea ikiwa na eneo kubwa kwa ajili ya matumizi binafsi ya wakazi ikiwa ni pamoja na maegesho ya magari hadi matatu

 

Taarifa kwa Umma: SWAHILI

 

Fomu ya Maombi(Bonyeza kuipata)

 

Utaratibu wa Ununuzi(Bonyeza kuipata)

 

Company Profile

The current NHC is the outcome of the decision of the Government to dissolve the Register of building (RoB) through Act of Parliament No.2 of 1990, which vested its responsibilities with the NHC.

Customer Start-up Kit
Contact Information
National Housing Corporation
P.O Box 2977,Dar es salaam-Tanzania
Hotline: 255 (754) 444 333
Fax: 255 (22) 285 1442
E-mail: sales@nhc.co.tz

 

NHC Facebook page and Youtube page